Maisha karibu na mgodi wa kobalti unaomilikiwa na Wachina nchini DRC
BBC News Swahili BBC News Swahili
600K subscribers
937 views
0

 Published On Premiered May 4, 2024

Christophe Kabwita anaishi umbali wa mita 500 tu kutoka katika mgodi unaomilikiwa na China ukichimbwa madini ya cobalt, nyenzo muhimu kwa uchumi wa kijani.

Anasema mgodi huo wa wazi, unaharibu maisha ya watu kwa kutumia vilipuzi kulipua mwamba huo mara mbili au tatu kwa wiki.

Ving'ora vya tahadhari hupigwa wakati ulipuaji unapokaribia kuanza, kama ishara kwa kila mtu kuacha anachofanya na kujificha.

Bw.Kabwita na wanakijiji wengine wamefichua hali mbaya ya maisha yao, iliyovurugwa na milipuko na uchafuzi wa mazingira ambao wanasema unasababishwa na mgodi huo.

#bbcswahili #DRC #mgodi

Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili    / @bbcnewsswahili  

show more

Share/Embed